Tumieni maziwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji

HomeKitaifa

Tumieni maziwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji

Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara zinazohusika na kilimo na uvivu kufanya mchakato wa kuvuta maji kutoka kwenye maziwa yaliyopo nchini ili yaweze kutumika kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Akishiriki kilele cha Sikukuu ya Nanenane iliyofanyika kitaifa jijini Mbeya, Rais Samia alitolea mfano wa nchi ya Misri na kusema ingawa wana jangwa, wanatumia maji ya Ziwa Nile kuzalisha ngano.

“Mungu ametubariki maziwa Victoria, tuna Nyasa , tuna Tanganyika, maji yako pale. Tukivuta maji machache kufanyia kilimo haitadhuru samaki walikuwepo pale wala haitapunguza kina cha maji cha meli kuelea kwenye hayo maziwa.” amesema Rais Samia.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia kwenye Kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya

Aidha, Rais Samia alimalizia kwa kuzihimiza mamlaka husika kufanya uchunguzi na kuchangamkia suala hilo ili kuwawezesha wakulima waweze kulima mara mbili kwa mwaka.

 

error: Content is protected !!