Abu Dhabi kuikopesha Tanzania mkopo wa bilioni 69.9 ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme

HomeKitaifa

Abu Dhabi kuikopesha Tanzania mkopo wa bilioni 69.9 ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), na Mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (Abu Dhabi Fund for Development), Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi, wameitia saini mkataba wa mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 30, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 69.9 za Tanzania, kwa ajili ya Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme Msongo wa kV 220, yenye urefu wa kilometa 167 kutoka Benaco hadi Kyaka, pamoja na Upanuzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kyaka mkoani Kagera.

Image

Tukio hilo limeshuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Mfuko huo, akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa Tanzania-Falme za Nchi za Kiarabu-Luteni Jenerali (Mstaafu) Yacoub Hassan Mohammed, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Bw. Maharage Chande, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje Bw. Rished Bade, Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justin, pamoja baadhi ya Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania UAE.

error: Content is protected !!