Walioathiriwa na ajali ya basi Mtwara kulipwa fidia

HomeKitaifa

Walioathiriwa na ajali ya basi Mtwara kulipwa fidia

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeiagiza kampuni ya bima ya Reliance ihakikishe waathirika wote wa ajali iliyoua watu 13 wakiwemo watoto 11 wanalipwa fidia kwa mujibu wa sheria baada ya taratibu za kipolisi na kibima kukamilika.

Pia Kamishna wa Bima nchini, Dk Baghayo Saqware ameagiza kampuni hiyo ishirikiane na familia zote zilizopoteza wapendwa wao.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Tira, Dl Saqware alisema basi hilo lilikuwa na bima hai na halali.

Dk Saqware alitoa pole kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, wafiwa wote na wananchi kwa ujumla kutokana na ajali iliyohusisha basi hilo la wanafunzi lenye namba za usajili T207 CTS.

 

error: Content is protected !!