Tunda aahirisha kujiua

HomeBurudani

Tunda aahirisha kujiua

Video vixen kutoka nchini Tanzania, Mkurugenzi na mmiliki wa duka la nguo za kike la Tunda Boutiques, Tunda Sebastian amesema hatajiua kama alivyosema kwamba mwaka huu 2021 ukiisha bila kuolewa basi atajiua, na badala yake amepeleka mbele mipango yake mpaka mwakani mwezi wa kumi na moja.

“Nilisema mwaka huu nisipoolewa najiua…kuna marekebisho ya kiufundi yamejitokeza nasogeza hadi mwakani mwezi kama huu. Kuna vitu vimeni inspire kwenye maisha ya usingle nimeona niendelee kubaki baki single,” ameandika Tunda.

Kupitia taarifa hiyo, Tunda amewaacha wengi na maswali kama bado yupo na mzazi mwenzako msanii Whozu ambapo hivi karibuni wawili hao walibarikiwa mtoto wao wa kwanza wa kike waliyempa jina la Lola au wameachana kama jinsi watu wanavyosema kutokana na wapenzi hao kutoonekana pamoja.

error: Content is protected !!