TPDC, CNOOC ya China kushirikiana katika sekta ya gesi

HomeKimataifa

TPDC, CNOOC ya China kushirikiana katika sekta ya gesi

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Kampuni ya China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) na Shirika la Maendeleo la Petroli la Tanzania(TPDC)yameahidi kushirikiani katika sekta ya gesi nchini.

Waziri Makamba alitoa taarifa hiyo wakati wa mkutano kati yake na Mwenyekiti wa Kampuni ya CNOOC, Bw. Wang Dong Jin ambaye ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau wengi katika uwekezaji wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Kusafirisha Mafuta kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Image

Kukamilika kwa mradi wa Bomba La Mafuta utaongeza mapato kwa serikali, kuzalisha ajira za muda mrefu ambapo zaidi ya ajira 10,000 zitapatikana.

error: Content is protected !!