China yaahidi kuwekeza sekta ya nishati Tanzania

HomeKitaifa

China yaahidi kuwekeza sekta ya nishati Tanzania

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Mfuko wa Uwekezaji wa China Africa Development Fund (CADFUND) umeonesha nia ya kuwekeza Tanzania katika sekta ya nishati kwa kupitia ushirikiano na makampuni ya Tanzania.

Mhe. Makamba alisema Mfuko wa CADFUND wenye mtaji wa Dola za Kimarekani Bilioni 15 uliazishwa na Serikali ya China kwa madhumuni ya kuwekeza katika miradi ya uwekezaji Afrika na kwa Tanzania mfuko huo umewekeza katika sekta za kilimo, sekta za viwanda na sekta ya mawasiliano ( kwa ubia na Kampuni ya Startimes na TBC).

Ushikirikiano wa Tanzania na China ni utekelezaji wa azma ya Rais Samia Suluhu katika kuhakikisha biashara na uwekezaji na teknolojia na ujuzi kwa Watanzania unakua.

error: Content is protected !!