Maji ya upako yaharibu sehemu zake za siri

HomeKitaifa

Maji ya upako yaharibu sehemu zake za siri

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Ummy Msika(45) mkazi wa kata ya Bomambuzi Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amedai kuharibiwa sehemu za siri na maji ya upako aliyopewa na rafiki yake ili ayatumie kuondoa miwasho iliyokuwa inamsumbua kwenye mapaja.

“Siku moja nilikutana naye (rafiki yake) akanipa yale maji nikanywa mafunda matatu, lakini pia akaniambia nikisikia nawashwa sehemu yoyote nipake yale maji nami nilifanya hivyo nikijua ninajitibu kumbe ndiyo naongeza matatizo,” alisema Ummy.

Ummy alileza kuwa baada ya kuyatumia maji hayo ndipo alipoanza kupoteza ladha ya chakula na kuanza kutoka na harahara kwenye maeneo anayowashwa na hata alipopaka maji aliendelea kuwashwa.

Aidha, mwanamke huyo ameiomba serikali kuyachunguza maji hayo ili kujua kama yalikuwa ni maji ya baraka ama kulikuwa na kitu kingine cha ziada kiliwekwa ili kuwadhuru watumiaji.

 

error: Content is protected !!