Diwani CCM apotea

HomeKitaifa

Diwani CCM apotea

Diwani wa Kata ya Kawe mkoani Dar es Salaam, Mutta Rwakatare (CCM) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha huku vyombo vya dola vikiombwa kushughulikia tatizo hilo.

Meya Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge alisema Diwani huyo hajaonekana muda mrefu na hajulikani alipo hivyo wanaviomba vyombo vya usalama kuingilia kati.

“Diwani mwenzetu hayupo nyumbani, mtaani. Ofisini wala Manispaa, lakini taarifa tulizoambiwa amefichwa sasa hatujui nani amemficha, tunamtaka huyo aliyemficha ajue anamnyima nafasi ya kwenda kuwahudumia wananchi,

“Tunamtaka amuachie mara moja kwani taarifa zinasema yupo basi kama yupo hotelini au chuo cha uchungaji tunaomba atoke mara moja aje kuwahudumia wananchi,” alisema.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai alisema wao wanasikia taarifa hizo mitaani na kwamba hawana taarifa rasmi iliyowasilishwa kwao.

“Tunasikia tu mtaani huko kama ambavyo na ninyi mmesikia, tunasubiri taarifa kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zake waje watuambie kwa taarifa ili na sisi tutoe taarifa,” alisema Kamanda Kingai.

error: Content is protected !!