Kesi ya Mange yafutwa

HomeKitaifa

Kesi ya Mange yafutwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubali kuondoa kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Mtandao wa U- turn unaoendesha App ya Mange Kimambi, Allen Mhina baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuomba iondolewe.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai DPP aliwasilisha hati ya kuonesha hana nia ya kuendelea na shauri hilo, hivyo aliomba Mahakama ikubali kuliondoa, mahakama ilikubali kuonda na kuwaachia huru washitakiwa.

Kesi hiyo, ilikuwa ikuhusu kurushwa kwa video ya mwanamuziki na aliyewahi kuwa mbunge wa Mikumi, Profesa J akiwa ikimuonesha akiwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi Hospitali ya Taifa Muhimbili ilitakiwa kusikilizwa Juni mosi mwaka huu.

Video hiyo iliyoonesha mgonjwa aliyekuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi iliambatana na maneno “PROFESA JAY AKIWA ICU. Hii ndiyo hali ya Profesa Jay kwa sasa tumuombee,” ikiwa ni maudhui yenye kudhalilisha na kukiuka haki za faragha.

 

error: Content is protected !!