Madhara ya kutumia simu bila kunawa mikono

HomeElimu

Madhara ya kutumia simu bila kunawa mikono

Mfamasia Erick Venant amesema simu za mkononi zimetajwa kuwa ni hatari katika kusambaza na kuhifadhi vijidudu vya magonjwa ya kuambukiza kama zitashikwa bila kunawa au baada ya kutoa huduma.

Aliyasema hayo alipokuwa akitoa mada ya uelewa na umuhimu wa unawaji mikono kwa watumishi wa afya Tanzania (THS) ikiwa ni miongoni mwa mada saba zilizotolewa na Mradi wa HPSS-Tuimarishe Afya unaotekelezwa na Shirika la Swiss TPH kwa ufadhili wa Shirika la Ushirikiano na Maendeleo la Uswisi (SDC).

Katika mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dodoma, Venant alisema asilimia 63 ya madaktari, wauguzi na wanafunzi walio kwenye mafunzo kazini, 270 waliofanyiwa utafiti kwenye mkoa huo walibainika wana uelewa kuhusu unawaji mikono kulingana na mwongozo wa WHO, huku asilimia 2,6 wamekuwa wakitekeleza kikamilifu mwongozo huo.

Aidha katika utafiti huo ulibani kuwa asilimia 34 ya simu za watumishi zilizotumika kama sampuli kwenye utafiti huo zilikuwa zina bakteria mbalimbali kama staphylococci ambao wana sugu, hivyo amesisitiza watoa huduma hao kuwa makini na kunawa mikono kabla na baada ya kutoa huduma

error: Content is protected !!