Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 19 (Unai Emery njia nyeupe kuelekea Newcastle, huku PSG ikifanya swap ya Icardi kumpata Aguero)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 19 (Unai Emery njia nyeupe kuelekea Newcastle, huku PSG ikifanya swap ya Icardi kumpata Aguero)

Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez, kocha wa Rangers Steven Gerrard na kocha wa Villarreal Unai Emery wanatajwa kuwa kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa kumrithi kocha Steve Bruce wa Newcastle United (Times). Newcastle kwa sasa imnadhamiria kuleta ushindani kwa timu kubwa katika ligi kuu ya England.

Paris St-Germain huenda ikamtoa mshambuliaji wake Mauro Icardi 28, kubadilishana na mshambuliaji Sergio Aguero 33 anayekipiga kunako klabu ya Barcelona ifikapo dirisha la usajili mwezi Januari (El Nacional). Dili hili huenda likatokea kutokana na Icardi kuonekana kukosa raha ndani ya PSG hivi karibuni.

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah 29, anataka mshahara wa £400,000 kwa wiki ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Anfield (Telegraph). Kutokana na makali yake anayoyaonyesha katika klabu yake na ligi kwa sasa ni moja ya sababu itakayiamsha Liverpool kupatia mshahara huo.

> Tetesi za Soka Ulaya  Oktoba 18

Manchester City ipo tayari kumuuza Raheem sterling 26, kwa dau la euro 80m mchezaji huyo kwa sasa anahusishwa na klabu ya Barcelona (Marca).

Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe 22, ambaye anawaniwa na Real Madrid, amegusia kwamba ana ndani ya klabu hiyo (Marca). Hili linatokea baada ya kuwepo na uvumi kwamba mchezaji huyo hana furaha pale alipogoma kusaini mkataba mpya na kushinikiza kuondoka.

Liverpool imetaarifiwa na Lazio kwamba bei ya kiungo Mserbia Sergej Milinkovic-Savic 26, inaanzia £67m (Calciomercato – Italian). Liverpool inamsaka mchezaji huyu kuja kuimarisha kikosi chao haswa kuwasaidia katika mashindano ya ligi kuu ya England na UEFA Champions League.

Klabu ya Arsenal na Leicester City vinamfuatilia winga wa Southampton Mohamed Elyounoussi 27, baada ya nyota huyo kuonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu (Sun).

Manchester United itachuana na Manchester City katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Real Sociedad na Sweden Alexander Isak, 22 (Fichajes – Spanish).

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer hajafurahishwa na klabu hiyo kushindwa kusajili kiungo katika dirisha lililopita la usajili (Manchester Evening News). Ni baada ya timu hiyo kutofanya vizuri katika ligi iliyopelekea hivi karibuni klabu hiyo kupoteza kwa kichapo cha goli 4 – 2 dhidi ya Leicester city.

Hamasa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ipo chini baada ya kipigo dhidi ya Leicester City kukiacha kikosi hicho cha Solskjaer kutoshinda mechi yoyote kati ya tatu zilizopota za ligi kuu (Times).

error: Content is protected !!