Japan kutoa Dola bilioni 30 za miradi, mazingira Afrika

HomeKimataifa

Japan kutoa Dola bilioni 30 za miradi, mazingira Afrika

Serikali ya Japan imeahidi kutoa dola za Marekani bilioni 30 (sawa na Sh 69.9 za Tanzania) kuziwezesha nchi za Afrika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuimarisha utunzaji wa mazingira.

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida alitoa ahadi hiyo jana akitoa hotuba kwenye mkutano wa nane wa kimataifa wa wakuu wa nchi na serikali unaohusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD8) uliofanyika jijini Tunis nchini Tunisia.

Akizungumzia kuhusu kiasi cha fedha kilichotelewa, Mhe. Fumio amesema kupitia mpango wa TICAD sekta binafsi za pande zote mbili (Japan na Afrika) zimeendelea kustawi, hivyo Serikali yake itaendelea kuhamasisha Kampuni za Japan kuendelea kuwekeza Afrika katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo, Afya, nishati ya umeme na teknolojia. 

Kuhusu mgawanyo wa fedha hizo Mhe. Fumio amesema kuwa pamoja na TICAD kufanikiwa katika maeneo mengi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya na elimu, Japan katika kipindi cha miaka miatatu ijayo (2022/23-24/25) itaangazia pia maeneo muhimu yanayogusa maisha ya watu ya kila siku. 

Ameyataja maeneo hayo kuwa ni mapinduzi ya kijani, Mabadiliko ya tabia nchi, kukuza uwekezaji, kuendeleza hali ya maisha ya Waafrika, ambapo kiasi cha Dola za Marekani bilioni 5 zitatolewa kufanikisha mpango huo. 

Akizungumza katika mkutano huo Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameeleza umuhimu wa Bara la Afrika kuendelea kushikirikiana na Jumuiya ya Kimataifa katika kutatua changamoto zinazolikabili bara hilo katika ukuzaji wa uchumi. 

Mhe. Mjaliwa akiongelea madhara yaliyo sababishwa na athari za UVIKO 19 na Vita vya Urisi na Ukraine ikiwemo mfumuko wa bei wa bidhaa, ametoa rai kwa Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika katika jitihada zake za kujigemea kiuchumi, ili kuhakikisha zinaendelea kutoa huduma bora na muhimu kwa wananchi wake na kuwawezesha wananchi katika shughuli zao zinazowagusa moja kwa moja kama vile kuendeleza kilimo na utalii.

 

error: Content is protected !!