Mambo matatu yakufanya unapopitia simu ya mpenzi wako

HomeElimu

Mambo matatu yakufanya unapopitia simu ya mpenzi wako

Kupitia simu ya mweza wako bila wao kujua ni makos, lakini mara nyingine inaweza kuwa na umuhimu.

Ikiwa unapata hisia ya mambo kutokwenda sawa na hivyo kuamua kupitia simu ya mpenzi wako, basi unapaswa kujiaandaa kwa mambo haya matatu.

Baki kimya

Jiandae kuwa kimya na kutosema chochote kuhusu mambo utakayoyakuta bila kujali ni kitu gani umeona kwenye simu ya mwenza wako.

Ikiwa umepitia simu ya mpenzi wako bila yeye kujua basi kubaliana na lolote utakalokutana nalo sababu inaweza kukusarisha. Waswahili wanasema kama huna kifua cha kuhifadhi mambo basi usithubutu kukagua simu ya mwenza wako.

Jianda kwa chochote

Chochote kinaweza kutokea na pia ukumbuke kwamba mwenza wako hawezi kukuambia kila kitu hivyo basi kuwa tayari kwa utakayokuta kwenye simu yake.

Ikiwa hauko tayari kwa vurugu au matokeo mabaya yanaweza kutokea, ni bora kuepuka kukagua simu ya mwenza wako.

Epuka kumkabili baada ya ukaguzi

Hiyo ni simu ya mwenza wako, sio yako, ikiwa utakuta mambo yanayokukera, acha kusoma na urudishe simu yake.

Ikiwa huwezi kudhibiti hisia zako, itakuwa bora kutopitia simu ya mwenzi wako kabisa.

Fahamu kwamba amani ya akili yako na utulivu wako ni muhimu. Kama unahisi mwenza wako anakupa mashaka basi keti naye chini mzungumze.

error: Content is protected !!