Pablo atemwa na Simba

HomeKitaifa

Pablo atemwa na Simba

Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco Martin.

Katika kipindi chake kocha Pablo ameiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kufika robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Katika kipindi chote cha kumaliza msimu, Simba itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Selemani Matola.

Pia, Klabu imefikia makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba na kocha wa viungo Daniel De Castro Reyes.

 

Older Post
error: Content is protected !!