Mwijaku ashinda kesi

HomeKitaifa

Mwijaku ashinda kesi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Mei 31 imemwachia huru Mwemba Burton maarufu Mwijaku ambaye alikuwa anakabiliwa na shtaka la kusambaza picha za ngono za Muimbaji, Menina.

Mwijaku na Menina enzi za mahusiano yao.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Rhoda Ngimilanga amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kwamba Mwijaku ndiye aliyesambaza picha hizo chafu.

Mtangazaji huyo wa clouds media almaarufu alikutwa na kesi ya kujibu ya mwaka 2019 baada ya kusemekana amehusika katika kusambaza picha za utupu za muigizaji na aliyewahi kuwa mpenzi wake Menina.

error: Content is protected !!