Rais Samia atunukiwa Tuzo Bodi ya Utalii Afrika

HomeKitaifa

Rais Samia atunukiwa Tuzo Bodi ya Utalii Afrika

Bodi ya Utalii Afrika (ATB), imemtunuku Rais Samia Suluhu Hassan tuzo ya Utalii kwa kutambua juhudi zake za kukuza sekta hiyo nchini. Tuzo hiyo ilitolewa jana Jijini Arusha katika maonesho ya utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EARTE) ambayo lengo lake ni kutangaza vivutio vya utalii na fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta hiyo.

> Rais akoshwa majengo ya mahakama kutenga maeneo kwa wanaonyonyesha

Mwenyekiti Mtendaji wa ATB, Cuthbert Ncube alikabidhi tuzo hiyo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro aliyepokea kwa niaba ya Rais Samia na kusema pamoja na changamoto za janga la irusi vya Korona, sekta ya utaliii imeanza kurejea hali yake ya kawaida kutokana na juhudi za Rais Samia. #clickhabari #utalii

error: Content is protected !!