Fahamu faida 6 za juisi ya nyanya kwa wanaume

HomeElimu

Fahamu faida 6 za juisi ya nyanya kwa wanaume

Nyanya ni tunda/kiungo linaloliwa na kutumiwa kwa njia mbalimbali. Wengine hutumia kutengenezea kachumbari, wengine huungia mboga, wengine hupikia rosti lakini wengine hupendelea kuisaga na kunywa juisi (juice). Tunda hili lina faida sana katika mwili wa binadamu, lakini zaidi ni kama litatumika likiwa na virutubisho vyake vyote, yaani likiwa bado bichi.

Nyanya mbichi ni chanzo cha Vitamin A, Vitamin K, Vitamin B1, B2, B3, B5 na B6, pamoja na madini kama magneziam (magnesium), chuma (iron) na fosforas (phosphorus).

Tafiti mbalimbali zimefanyika na kugundua kuwa, nyanya hasa katika mfumo wa maji ama kimiminika (liquid), ina faida. Moja kwa moja tuziangalie faida za juice ya nyanya kwa ngozi, nywele na afya ya mwili.

Juisi ya nyanya ni kusaidia kupunguza uzito uliopitiliza na kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu ya mtumiaji wa juisi ya nyanya.

Juisi ya nyanya husaidia kuboresha mbegu za uzazi kwa wanawake na wanaume wenye umri unaoruhusu masuala hayo. Wanawake na Wanaume (wote) wakinywa juisi hii, hupata viini lishe vya kuwaongezea virutubisho kwenye mbegu za kiume na mayai ya wanawake ambavyo mwishowe husaidia kuzaliwa mtoto asiye na matatizo.

Zifahamu faida za bamia kwa wanawake

Juisi ya nyanya husaidia kuimarisha nywele, hasa zile nyepesi kwa kuzifanya kuwa nzito. Nyanya imejaaliwa kuwa na virutubisho vingi kama vitamin C, A na K, madini ya Potassium, Manganese, Chromium, Vitamin B1 na Vitamin B6. Virutubisho hivi vinahusika katika ukuaji wa kucha na nywele.

Juisi ya nyanya huimarisha afya ya mifupa ya watumiaji na kusaidia kupunguza maumivu ya mwili.

Juisi ya nyanya humpunguzia mlaji uwezekano wa kupata saratani mbalimbali ikiwamo za tezi dume, saratani ya utumbo, saratani ya kizazi kwa wanawake, ya koo na mdomo na mapafu.

Juisi ya nyanya husaidia kuimarisha ngozi na kuifanya nyororo na kusaidia uso kuondokana na mikunjo na chunusi.

error: Content is protected !!