Njia 3 za kuvutia wateja kwenye biashara yako

HomeBiashara

Njia 3 za kuvutia wateja kwenye biashara yako

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu kupotea kwa wateja wao mara anunuapo bidhaa kwake, wengine ufikia mpaka kuhisi kama kuna imani za kishirikina zinatumika kuwaondoa wateja hao lakini wanashindwa kutambua kwamba mchawi anaemtafuta ni yeye mwenyewe.

Unaweza kuwa mtoa huduma bora kwa wateja wako endapo utazingatia mambo yafuatayo:

1. Tumia lugha chanya.
Epuka kutumia lugha hasi kwa wateja wako, endapo kitu kimeisha usiseme “ hicho hakipo labda uje wiki ijayo,” badala yake mwambie “kwa sasa hamna lakini tumeagiza mzigo upo njiani,” kauli kama hii itampa mteja moyo wa kurudi tena kwani umeshampa uhakika wa kuja kwa bidhaa hiyo.

2. Toa ushauri wa bure kwa mteja wako.
Endapo unaona ananunua kitu ambacho unajua hakitamfaa basi ni vyema ukamshauri achukue kitu kingine kitakachomfaa, kwa kufanya hivyo mteja anaweza kurudi tena siku nyingine na hata kukuletea wateja wengine.

3. Toa huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya mteja wako
Hakikisha bidhaa zako zina ubora na zinakidhi mahitaji ya wateja wako, kwani ukiwa na bidhaa bora wateja watakuwa wanakuja kwako na kuongezeka mara dufu.

Kama mtoa huduma au mfanyabiashara utazingatia njia tajwa hapo juu basi utaweza kufanya wateja wako waruke na kuacha maduka mengine na kuja kwako.

error: Content is protected !!