Serikali: Wafanyabiashara wadogo watengewe maeneo yanayofikika

HomeKitaifa

Serikali: Wafanyabiashara wadogo watengewe maeneo yanayofikika

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa kuzisimamia Halmashauri nchini ili kuhakikisha zinaandaa maeneo mazuri yanayofikika na wateja kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la 5 la uwezeshaji lilloandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

“Tumeagiza Halmashauri zetu kuandaa maeneo mazuri ya kufanya ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Sio kila eneo linalofaa kwa biashara. Ni maeneo mazuri, yanayofanya biashara na wateja wakafika kupata huduma hiyo,” amesema.

Pia amewataka wafanyabiashara wadogo kushirikiana na Serikali kama inavyofanyika kwa machinga kupata maeneo mazuri ya biashara.

error: Content is protected !!