Mama aua watoto wake kisa ugumu wa maisha

HomeKitaifa

Mama aua watoto wake kisa ugumu wa maisha

Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia huku wengine watatu wakinusurika kifo baada ya kunyweshwa sumu na mama yao mzazi, Veronica Gabriel mkazi wa kijiji cha Mwabagaru kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Tukio hili lilitokea Desemba 2 katika kijiji cha Mwabagaru ambapo Veronica baada ya kuwanywesha watoto wake sumu, naye akanywa sumu kwa lengo la kujiua kwa madai ya kuelemewa na ugumu wa maisha.

“Mwenyekiti naye alipata taarifa kutoka kwa watu waliokua wamepita jirani na nyumba hiyo na kusikia harufu kali ya dawa ya kuua wadudu kwenye pamba na ndani ya nyumba kukawa kama kuna kelele, wakaamua kuingia ndani na kukuta tayari mama huyo ameshawapa sumu watoto wake na kunywa yeye mwenyewe. Ndipo wakampigia simu mwenyekiti” alisema diwani Buseresere Godfrey Miti akiwa anaelezea jinsi taarifa zilivyowafikia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe, alisema mwanamke huyo mwenye watoto watano aliwanywesha sumu ya kuulia wadudu kwenye nyanya aina ys incecron profenos 720/L na kusababisha vifo vya watoto wake wawili.

“Wakati mwanamke huyo akinusurika kifo baada ya kunywa sumu hiyo kwa lengo la kujiua, watoto wake wenye umri kati ya mwaka mmoja na miezi tisa na mwingine mwenye miaka 12 walipoteza maisha kwa kunyweshwa sumu” alielezea kamanda Mwaibambe.

Watoto watatu walionusurika kifo wako katika kituo cha afya Bwanga, huku mama yao akiwa chini ya ulinzi polisi akisbiri uchunguzi ukamilike ili hatua za kisheria zichukuliwe.

error: Content is protected !!