Rais Samia: Hii ndio Tanzania ninayoitaka

HomeKitaifa

Rais Samia: Hii ndio Tanzania ninayoitaka

Rais Samia Suluhu Hassan anatimiza mwaka mmoja tangu achukue madaraka ya nchi, pamoja na maendeleo anayosimamia amebainisha mikakati yake muhimu na Tanzania anayoitaka.

Akizungumza kwenye mahojiano na Bakari Machumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd- wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na Mwananchi Digital, Rais Samia alisema kwamba anataka kuona Tanzania ambayo ina watanzania wanaojielewa kwa kuilinda Tanzania na kuitumikia vyema.

“Ningependa kuona Tanzania ambayo ina Watanzania wanaojielewa kama nilivyosema mwanzo, kwamba wao ni Watanzania , utaifa wao ni Utanzania na wana wajibu kuitumikia Tanzania na kulinda mali za Tanzania,”

“Lakini ningependa kuona Tanzania inayodumisha amani na utulivu kama tulivyo hivi. Tanzania ambayo imeshamiri na siasa zinafanywa kwa ustaarabu, hiyo ndiyo Tanzania ambayo ningependa mimi kuiona inakua kiuchumi, demokrasia inashamiri,siasa za kistaarabu, kila mtu yuko happy (ana furaha) ana amani ya moyo,” alisema Rais Samia Suluhu.

Aidha, Rais Samia aliongeza kwa kusema angependa kuona Tanzania ambayo wananchi wake hawakosi mahitaji muhimu kwa siku kama chakula huku akikiri kwamba mabadiliko hayo hayawezi kuja ndani ya miaka mitatu labda miaka mitano, saba au hata kumi.

error: Content is protected !!