Poland yatwaa taji Miss World

HomeKimataifa

Poland yatwaa taji Miss World

Miss Polonia (Poland) 2019, Karolina Bielawska, ameibuka mshindi wa mashindani Miss World 2021yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo huko Puerto Rico.

Bielawska anatwaa taji hilo kutoka kwa Toni-Ann Singh wa Jamaica ambaye ndiye Miss World aliyeweka historia ya kulivaa taji kwa muda mrefu zaidi.

Mshindi wa pili (1st Runner up) ni Shree Saini kutoka Marekani, na mshindi wa tatu (2nd Runner Up) ni muafrika Olivia Yace wa Cote d’Ivoire.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Miss World (@missworld)

Jumla ya washindani 98 walikutana kwaajili ya kukiwania kiti hicho.

Mshiriki wa kwanza kuvaa hijabu kwenye mashindano ya Miss World ni Khadija Omar kutoka Somalia ambaye alikuwa kati yawashiriki 40 bora

Mashindano ya Miss World 2021 yaliahirishwa kutokana na uwepo wa ugonjwa wa UVIKO-19

Mashindano haya ni mashindano ya 70 ya Miss World.

 

error: Content is protected !!