Tommy Flavour afunguka madai ya kuiba wimbo na kumpa Alikiba

HomeBurudani

Tommy Flavour afunguka madai ya kuiba wimbo na kumpa Alikiba

Mwandishi na mwimbaji kutoka lebo ya Kings Music, TomyFlavour amefunguka na kusema mashtaka kuhusu kuiba wimbo wa mwanadada anayefahamika kama Liah na kumpa Alikiba sio kweli kwani yeye aliuandika wimbo huo miaka 5 iliyopita.

“Nachoweza kusema ni uongozi unafatilia hilo suala lakini hakuna ukweli wowote kuhusiana na yeye kumiliki huo wimbo kwa sababu ni wimbo ambao nilishaufanya miaka mitano nyuma iliyopita na siwezi kumdhulumu wimbo mtu,” amesema Tommy Flavour.

> Jela miaka mitano kwa kuuza albamu ya Alikiba mtaani

Wimbo unaodaiwa kuibwa upo kwenye albamu ya Alikiba unaokwenda kwa jina la Sitaki Tena, huku mwanadada Liah akisema wimbo huo ni wa kwake unaitwa Doa.

Kwa upande wa mtayarishaji wa nyimbo zilizomo kwenye albamu ya Ali Kiba, Yogo Beats amesema kuhusiana jambo hili ni vyema akatafutwa mtayarishaji wa nyimbo Clouds Beat kwani yeye alishafanya kazi na Tommy flavour pamoja na mwanadada huyo Liah.

error: Content is protected !!