Jela miaka mitano kwa kuuza albamu ya Alikiba mtaani

HomeKitaifa

Jela miaka mitano kwa kuuza albamu ya Alikiba mtaani

Ofisa Mtendaji Mkuu na msimamizi wa hatimiliki kutoka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Doreen Anthony Sinare amekemea vikali watu wanaouza mtaani albamu ya Alikiba iliotoka hivi karibuni “Only One King.”
 
Bi. Sinare amesema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na adhabu yake inaweza kuwa faini shilingi milioni 20 au jela miaka mitano kwa mujibu wa sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki namba 7 ya mwaka 1999.
 
Albamu ya Alikiba ambayo yeye alitangaza itakuwa inapatikana kwenye majukwaa ya mtandaoni, imeanza kuuzwa mitaani kwa watu kuchukua albamu hiyo mtandaoni na kutengeneza diski ndogo zinazosambazwa mitaani bila makubaliano ya mwenye mali.
 
Only One King imefanikiwa zaidi baada ya kufikisha wasikilizaji milioni moja kutoka kwenye jukwaa la kusikiliza muziki linalojulikana kama Boomplay, na kushika namba moja katika jukwaa la kusikiliza nyimbo la Apple Music nchini Tanzania.
error: Content is protected !!