Vigogo Dar wawekwa kitimoto

HomeKitaifa

Vigogo Dar wawekwa kitimoto

Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amethibitisha kuwamba wapo watendaji waliosimamishwa kazi ili kupisha kwa uchunguzi wa ufisadi wa mamilioni ya shilingi.

Amewataja waliosimamishwa kazi ni Mhazini TRulusuba Kamalamo, Mhasibu Mkuu wa Mapato James Bangu, Msaidizi mkuu wa mhasibu wa Mapato Deogreatius Rutataza, Mtunza fedha mkuu Abdala Mlawe na Ofisa Masoko Mkuu Burhani Kaisi.

Tayari Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeanza kufanya ukaguzi huo maalumu kubaini upotevu wa fedha hizo za mapato yaliyokusanywa kupitia mashine za POS. Uchunguzi huo umekuja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu  kutilia shaka ukusanyaji nmapato wa robo ya kwanza ya mwaka 2021/2022 ambayo ni asilimia 26 ya lengo.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amesema, watumishi hao wamesimamishwa ili kupisha uchunguzi na sio kwa tuhuma za wizi kwani hawawezi kuendelea kufanya kazi huku kuna uchunguzi maalum unafanywa na CAG, ilibainiushwa kuwa ukaguzi huo ukiisha watarudi kazini kuendelea na majukumu yao.

Utaratibu wa kutumia mashine za POS kukusanya mapato zilianza kutumika mwaka 2004, kwa maana ya kukusanya mapato kwa njia ya kieletrioniki tofauti na ule wa zamani wa kutumia ma Cashier. Ila kuna tuhuma za upotevu wa mapato zimeibuka kwa  sababu kuna ujanja unafanyika kwa ushirikiano wa watu wa wanaokusanya fedha na watu wa IT.

error: Content is protected !!