Shilole: endelea ‘kujaji’ mwili wangu

HomeBurudani

Shilole: endelea ‘kujaji’ mwili wangu

Msanii wa kike wa bongo fleva Zuwena Yusuf maarufu kwa jina la kisanii Shilole au Shishi Baby anayetamba na wimbo wake wa Amsha Popo, amewataka wanaoendelea kumsema kuhusu mwili wake waendelee lakini wakumbuke kupambania maisha yao pia.

“We endelea kujaji mwili wangu shauri yako!! Pambania maisha yako kwanza,” ameandika Shilole.

Hivi karibuni watu wamekuwa wakimuandama Shilole kuhusu mwili wake kuwa mnene na wengi wakimtaka apungue lakini yeye mwenyewe anawajibu kwa kuwaambia kwamba yupo sawa na waache kumsema kuhusu umbo lake hili la sasa.

Shilole ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa instagram ambapo ameweka video ikimuonyesha akiimba kwenye kipindi cha Big Sunday Live (cha kituo cha televisheni ya Wasafi) siku ya Jumapili huku akimalizia kwa kuuliza watu kwamba “nani alisema mwanamke kibonge hawezi show?”

error: Content is protected !!