Diamond: Niliomba nisishiriki

HomeBurudani

Diamond: Niliomba nisishiriki

Msanii na mmiliki wa lebo wa Wasafi, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka na kueleza kwanini hayupo kwenye Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) baada ya kuulizwa na waandishi wa habari usiku wa jana alipokuwa kwenye hafla ya kuzindua video zake  10 za EP yake ya FOA.

“Mimi binafsi kwa heshima yangu, kwa harakati zangu na mikakati yangu ambayo ninayoipanga niliomba nisishiriki kwa sababu nafikiri kwanza nifocus na kushambulia kule, nikishatusua kule nataka wanamuziki wote wa Tanzania twende tukashambulie tuzo za kule kwahiyo niliomba. Naomba tukazi-support tuzo zimewekwa kwa nia njema, nia zilete chachu ya wanamuziki soko la ushindani lifanyike,” alisema Diamond.

Diamond pia amewasihi wanamuziki wenzake waweke ushindani kwenye kazi zao za sanaa na kushikana mikono kama wasanii kutoka Tanzania.

“Lazima tupigane kiakili tusifanye vita vya kiuendaazimu, wale wenzetu wanapigana kiakili , mbele kama wanapigana ila wakirudi nyuma marafiki ndomaana kwenye show zao wapo pamoja…wanatutengenezea tension yakutushambulia sisi wanamuziki wa Tanzania kwahiyo sisi tusipigane vita vya ukweli yani tusichukieane kiukweli ukweli, tufanye kinafki lakini nyuma tuwe marafiki sometime kwenye show tunaalikana ndoivyo,” alisema Diamond.

 

error: Content is protected !!