Rais Samia akiri kwamba Harmo ni Tembo

HomeKitaifa

Rais Samia akiri kwamba Harmo ni Tembo

Rais Samia Suluhu Hassan amemwagia sifa msanii Harmonize maarufu kama Konde boy au Tembo wakati akishiriki Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa mkoani Arusha, tukio ambalo lilihudhuriwa na wasanii wengine kama Marioo na viongozi mbalimbali wa nchi.

“Nimemuona pia Konde Boy Tembo hapa (kwenye orodha ya Wasanii waliotoa burudani) na kwa kifua kile cha Harmo kweli yeye ni Tembo. Kwa vikundi vyote vingine vilivyopanda hapa jukwaani kwa Burudani tunawashukuru kwa ujumbe kuhusu upunguzaji wa ajali za Barabarani,” amesema Rais Samia.

Katika hotuba yake Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi  kutoma elimu ya usalama wa barabarani kwa waendesha pikipiki (bodaboda) na kuwaelewesha nini wanatakiwa kufanya wakiwa barabarani kwani takwimu zinaonyesha kwamba ajali nyingi za barabara zinatokana na waendesha pikipiki.

Aidha , Rais amewasihi wananchi kuwa makini pindi watumiapo barabara na kuhakikisha wanazingatia alama za barabarani huku akisema jukumu la kuhakikisha usalama barabarani ni letu sote na linaanza na kila mmoja.

error: Content is protected !!