Hamisa Mobetto awajia juu walimwengu

HomeBurudani

Hamisa Mobetto awajia juu walimwengu

Mwanamitindo na msanii kutoka nchini Tanzania, Hamisa Mobetto ameandikia ujumbe mzito kwa watu wanaomsema vibaya kwenye mitandao ya kijamii na kumzushia maneno ya uongo kila kukicha, akiwataka watu hao kuacha tabia hiyo kwa kile alichoeleza kukerwa na tabia hizo.

“Na muache kunitungia story jamani mimi mwenyewe staring nakua sijui hiyo movie nimeicheza wapi na saa ngapi,  punguza story za kutunga maana soon utaonekana umechanganyikiwa , kama hauna kizuri cha kuongea bora ukapiga kimya. Na marufukuu kuandika story zangu kama huna proof,”ameandika Hamisa.

Pia Hamisa ameeleza kuchukizwa na jinsi watu wanavyounganisha picha zake na za wanaume ambao kwa upande wake amesema hana ukaribu nao hivyo waache hiyo tabia.

“Ifike mahala muache kuunganisha picha zangu na wanaume ambao sina ukaribu nao wala kufahamiana vizuri, tuheshimiane tafadhali inachosha kila siku kukuta picha zangu zinaunganisha ovyo, najua mnataka promo mfanye matangazo lakini punguzeni story za uongo kila kukicha.” ameandika Hamisa.

error: Content is protected !!