Kim na Kanye wageuka paka na panya

HomeBurudani

Kim na Kanye wageuka paka na panya

Mwanamitindo Kim Kardashian na rapa Kanye West ambapo awali walikua kwenye mahusiano na kubarikiwa kupata watoto wanne, North, Psalm, Chicago na Saint wamegeuka kuwa paka na panya kwa jinsi wanavyotupiana maneno mtandaoni.

Vita hiyo imeanza baada ya Kanye kuweka picha ya binti yake North kwenye ukurasa wake wa Instagram nakuuliza achukue hatua gani kwa kuwa mtoto wake amewekwa kwenye video za mtandao wa Tiktok bila ridhaa yake na mara baada ya ujumbe huo Kim naye hakukaa kimya akamjibu na kumwambia yupo kwenye uangalizi mzuri hivyo hakuna shida.

Sheria za mtandao huo wa Tiktok ni kwamba mtu anaweza kujiunga na kuutumia endapo atakuwa na miaka kuanzia 12 , jambo ambalo limemfanya Kanye West aanze kuhoji kwanini binti yake ameanza kutumia wakati ana miaka 8.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by ye (@kanyewest)

Bado Kanye hakutaka kuelewa ni nini mzazi mwenzake anasema na kwenda zaidi kudai kwamba Kim amekua akimnyima haki yakuwa karibu na watoto wake na kufika hatua yakusema kwamba anatumia madawa ya kulevya hivyo hapimwe.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by ye (@kanyewest)

Wawili hao wapo katika mchakato wakupeana talaka lakini kwa mujibu wa Kim ni kwamba Kanye amekuwa akiweka vipingamizi vingi na kufanya talaka hiyo kutotolewa kwa wakati.

 

error: Content is protected !!