Vaa hivi ufanane na Wizkid

HomeBurudani

Vaa hivi ufanane na Wizkid

Mwanamitindo wa Wizkid anastahili pongezi kwani tumeshuhudia mabadiliko ya mtindo wa uvaaji wake kutoka kwenye suruali za jeans chini ya makalio na mashati ya shingo ya mviringo hadi kuwa na muonekano wa mtindo na maridadi zaidi.

Siku hizi tunamuona Wizkid akiwa amevaa nguo kutoka kampuni kubwa za mitindo  za Marekani kama Prada, Louis Vuitton na Gucci ambazo zinagharimu pesa nyingi sana.

Hapa kuna vidokezo vya mitindo ya Wizkid;

  1. Vaa sweta zuri

 

View this post on Instagram

 

A post shared by BIG WIZ? (@wizkidayo)

Kuna uhusiano mzuri sana kati ya Wizkid na masweta hivyo kama unataka kuvaa kama yeye hakikisha sweta lako halikubani.

 

  1. Vaa shati na suruali zilizoachia

 

View this post on Instagram

 

A post shared by BIG WIZ? (@wizkidayo)

Ukitaka kufanana na nyota huyo kutoka Nigeria basi vaa shati na suruali ambazo zinaachia hazikubani kwani siku hizi Wizkid ameonekana akipendelea sana mtindo huu wa uvaaji.

  1. Vaa jaketi za wabunifu

 

View this post on Instagram

 

A post shared by BIG WIZ? (@wizkidayo)

Hakikisha unavaa jaketi za watu wabunifu wa mavazi, Wizkid anapendelea kuvaa jaketi kutoka kwa wabunifu kama Gucci, Prada na Tom Ford.

  1. Viatu vya wazi

 

View this post on Instagram

 

A post shared by BIG WIZ? (@wizkidayo)

Wizkid hupendela kuvaa viatu vya wazi vizuri na hivi humpa muonekana mzuri zaidi, hivyo kama unapendelea kuvaa kama yeye hakikisha unavaa viatu vya aina hiyo.

  1. Mashati makubwa

 

View this post on Instagram

 

A post shared by BIG WIZ? (@wizkidayo)

Hupenda pia kuvaa mashati makubwa yaliyoachia na uvaaji huo humpa muonekana mzuri zaidi bila kusahau kuvaa miwani nyeusi na vito vya dhahabu kama heleni, mkufu na saa ya mkononi.

 

error: Content is protected !!