Fahamu faida 4 za kununua nguo za mtumba

HomeElimu

Fahamu faida 4 za kununua nguo za mtumba

Nguo za mtumba ni zile ambazo tayari zimekwisha tumika na mtu au watu wengine sehemu nyingine na kuuzwa tena kwa ajili ya matumizi mengine. Watu wengi wamekuwa wakizidharau na kudharau watu wanaovaa nguo hizo kwa kuwa na fikra kwamba hununuliwa na kuvaliwa na watu masikini.

Lakini ukweli ni kwamba, nguo za mtumba zina faida kubwa kwetu na kwa mazingira kwa ujumla na baadhi ya umuhimu wa aina hizo za nguo ni;

  1. Zinaokoa  fedha

Moja wapo ya faida ya nguo za mtumba ni kwamba huokoa fedha kwani zinauzwa kwa bei nafuu sana. Huitaji kiasi kikubwa cha fedha ili uweze kununua nguo za mtumba kwani bei zake ni za chini na kila mtu anaweza kununua.

  1. Zinasaidia utunzaji wa mazingira

Aina hii ya nguo hutunza mazingira kwani zinafanya nguo ziwe kwenye mzunguko hivyo kusababisha nguo mpya zisizalishwe tena na kuokoa mazingira kutoka kwenye madhara ambayo yangetokea kwenye utengenezaji wa nguo mpya.

  1. Unapata nguo nzuri zisizofanana

Tofauti na nguo za madukani ambazo zinafanana, nguo za mtumba ni nzuri, zinakaa muda mrefu, hazichakai haraka  na pia huwezi kutoa zinafanana kama zile za kwenye maduka.

  1. Zinauzika tena 

Faida nyingine ya nguo hizi ni kwamba, endapo wewe ni mtunzaji mzuri wa nguo na ukanunua nguo hizi unaweza kuvaa na baadae ukizichoka unaweza kwenda kuziuza tena na wewe kununua nyingine.

 

error: Content is protected !!