Wanaopinga maboresho bandarini wanania tofauti

HomeMakala

Wanaopinga maboresho bandarini wanania tofauti

Nimejaribu kukumbuka matukio machache ya awamu zilizopita ya maamuzi ya Marais wa awamu zote kuhusu uwekezaji, na kuona kama kuna awamu yoyote wapinzani na wanaharakati walipinga tena kwa kupotosha

Nimekumbuka mwaka 1968 Nyerere alipoleta Wachina kujenga kiwanda Urafiki kwa mkataba ambao hauko wazi hadi kesho na wala Bunge halikupata ushiriki.

Then nikakumbuka enzi za Mwinyi wakati wa ruksa na kuanza kwa ubinafsishaji mwingi bila hata Bunge kuhusika.

Nikawaza zama za Mkapa, mzee wa cheni ya gold shingoni ambaye alipiga kazi na kubinafsisha hadi kuuza mali nyingi tu za umma kama nyumba za serikali.

Halafu nikawaza awamu ya Kikwete, ambaye aliwapa TICTS mkataba wao wa kwanza kuendesha Bandari ya Dar wakadumu nao kwa miaka 22 kukiwa na ukimya mkuu kama panya wanapotafuna godoro.

Kisha nikamkumbuka Magufuli a.k.a Jiwe ambaye alinunua ndege bila hata Bunge kupewa ruhusua ya kuhoji.

Then mwisho nikatafakari hii hatua ya Samia kufanya mabadiliko yenye tija bandarini (TICTS wamekiri kuwa wanahitaji mbadala).

Nikawaza mbona leo wanaharakati na wasiasa wameamka. Nikakumbuka kuwa ni vita ya maslahi, kuna kula ya watu inaenda kwisha, wanaipigania. Ni vita ya jinsia, hawajawahi kukutana na mwanamke shupavu, awamu zote wamekutana na wanaume. Vita hii naamini SSH kakusudia kushinda. Ndio sababu utafiti wa Afrobarometer unaonesha wanaokubali propaganda dhidi ya jambo hili asilimia 80% ni wanaume. Mshindi wa vita hii ni Watanzania wanaosimamiwa maono yao na Rais wao anayejua nini wanahitaji na namna watakifikia.

Husna Churi
Kilwa Masoko

error: Content is protected !!