Dar es Salaam jiji la 6 kwa usafi Afrika

HomeKitaifa

Dar es Salaam jiji la 6 kwa usafi Afrika

Rais Samia amesema kwamba jarida la Africa Tour Magazine, limelitangaza jiji la Dar es Salaam, ni Jiji la sita kwa usafi barani Afrika, ambapo katika utambulisho wake akatumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa mkoa huo kwa kusimamia usafi.

Rais Samia ametoa kauli hiyo hii leo Julai 12, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya miaka 20 ya AMECEA.

“Tanzania tumetiwa moyo sana kwamba jiji la Dar es Salaam, limetangazwa na jarida la Africa Tour Magazine kuwa ni jiji la sita kwa usafi Barani Afrika, na tumetoka mbali kwa wale wanaoikumbuka Tanzania miaka ya nyunma tulikuwa na vijibanda na miamvuli kila pahali,” amesema Rais Samia. 

 

 

error: Content is protected !!