Rayvanny aondoka rasmi WCB

HomeBurudani

Rayvanny aondoka rasmi WCB

Raymond Shaban Mwakyusa maarufu kama Rayvanny, ametangaza rasmi kutoa kwenye lebo ya muziki ya Wasafi inayomilikiwa na msaani Diamond Platnumz ikiwa ni takribani miaka 6 tangu ajiunge na kundi hilo lililomfungulia njia ya safari ya muziki.

Rayvanny ameamua kutoka na kwenda kuanzisha lebo yake ya Next Level Music aliyoitangaza hivi karibuni huku akikiri kwamba WCB imemkuza vyema na kumsaidia kuanzisha kampuni hiyo.

Akiwa WCB, Rayvanny ndio msanii wa kwanza kushinda tuzo kubwa za MTV, kupanda steji kubwa kama Dubai Expo na mafanikio mengi ambayo anakiri bila Diamond Platnumz kumpa nafasi asingeweza kufika mbali.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by CHUI… ? (@rayvanny)

error: Content is protected !!