Bwawa la Nyerere kujazwa maji leo

HomeKitaifa

Bwawa la Nyerere kujazwa maji leo

Rais Samia Suluhu Hassan leo atazindua ujazaji maji katika bwawa la kufua umeme kwenye Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) uliopo Rufiji mkoani Pwani, baada ya hatua ya kujenga tuta linalosaidia uhifadhi wa maji katika bwawa hilo kukamilika.

Rais Samia atafanya uzinduzi huo katika hafla itakayofanyika eneo la mradi kwa kubonyeza kitufe kitakachoshusha mageti yatakayoziba njia ya mchepusho wa maji na kuruhusu maji kuanza kujaa katika bwawa.

Hatua hiyo ya kujaza maji katika bwawa hilo lenye ukubwa wa meta za ujazo 32.3, inatarajiwa kutumia misimu miwili ya mvua kukamilisha kujaa na kuruhusu kuwashwa kwa mitambo ya kufua umeme.

Mradi huo unaotarajiwa kufua megawati za umeme 2,115, unatarajiwa kuondoa tatizo la uhaba wa uemme nchini na kupunguza gharama kwa wananchi.

Ongezeko hilo la megawati 2,115 litawezesha Tanzania kujitosheleza kwa mahitaji yake ya umeme na kuwa na ziada ya kuuzwa nje ya nchi.

error: Content is protected !!