Waliovamia ikulu ya Sri Lanka wakamatwa

HomeKitaifa

Waliovamia ikulu ya Sri Lanka wakamatwa

Serikali ya Sri Lanka, inakabiliana na baadhi ya viongozi wa waandamanaji walioandaa vuguvugu lililomwondoa madarakani rais wa nchi hiyo mwezi uliopita, huku ikiwakamara raia watatu akiwemo aliyeiba kikombe cha kunywea bia na aliyekalia kiti cha Rais.

Katika mpango huo, tayari Wanaharakati wakuu wamekamatwa, akiwemo Joseph Stalin, kiongozi wa chama cha walimu, na Mahanama Thero, mtawa wa Kibudha huku wengine wakipigwa marufuku ya kusafiri huku Serikali ikiamuru kuondolewa kwa mahema ya mwisho ya maandamano yaliyosalia.

Mwanaharakati na kamishna wa zamani wa haki za binadamu nchini Sri Lanka, Ambika Satkunanathan amesema Serikali ilikuwa ikiwawinda watu kwa makosa madogo ili kukomesha upinzani.

Waliokamatwa ni pamoja na muandamanaji anayedaiwa kuiba bendera rasmi ya rais, mwingine anayeshtakiwa kwa kuiba kikombe chake cha bia, na watatu ambaye anayesemekana alikalia kiti chake.

 

error: Content is protected !!