Rais Samia azindua mradi wa maji Mbalizi

HomeKitaifa

Rais Samia azindua mradi wa maji Mbalizi

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa maji wa Shongo- Mbalizi uliopo mkoani Mbeya ambao umegharimu zaidi ya Sh3.3 bilioni na utahudumia zaidi wa wakazi 80,000 katika eneo hilo.

Rais ameanza ziara ya siku tatu mkoani Mbeya leo Ijumaa Agosti 5,2022 ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa huo ikiwamo ya maji, afya, elimu na kilimo.

Akizungumzia na wananchi wa Mbalizi, Rais Samia amewataka wananchi kuutunza mradi huo ili maji yaendelee kupatikana na kuwataka watendaji wa taasisi za maji kuhakikisha maji yanapatikana kwa sababu serikali inatoa fedha nyingi kwenye miradi ya maji.

“Maji haya yamepatikana kwenye chanzo pale, ni matumaini yangu kwamba mtalinda kile chanzo. Ulinzi sio jukumu letu, ni jukumu lenu wananchi. Mkiona watu wanaharibu chanzo kile, wawajibisheni kwa sheria mlizojiwekea. 

 

“Niwamombe sana watendaji wa taasisi za maji, maji yaisikosekane. Serikali inaweka fedha nyingi sana kuhakikisha maji yanapatikana. Kama maji yatakatika, toweni tangazo kwamba maji yatakatika pengine kwa sababu ya matengenezo,” amesema Rais Samia.

Amewataka wananchi kuendelea kufanya kazi ya uzalishaji kwa sababu serikali inakusanya mapato yake kutoka katika shughuli zao na fedha hizo ndiyo zinatumika kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Wananchi tuendeleze uzalishaji, mapato ya serikali yanatokana na uzalishaji wenu. Sisi serikali tunakusanya kodi na tozo kutokana na shughuli mnazozifanya. Na kodi hizo ndiyo zinaleta maji, barabara, umeme, afya na elimu,” amesema Rais Samia.

 

error: Content is protected !!