Maisha ya Wasomali matatani Baada ya kifo cha waziri wa Uingereza

HomeKimataifa

Maisha ya Wasomali matatani Baada ya kifo cha waziri wa Uingereza

 

Mwakilishi wa Baraza la Mashirika ya Wasomali (CSO) Charlotte Gallagher amesema kwamba Wasomali na watu wenye asili ya Kisomali wamekua wakipokea vitisho vya kuuawa, baada ya kifo cha Mbunge Sir Alex Amess aliyeuawa kwa kuchomwa visu katika tukio ambalo Polisi nchini Uingereza walisema ni la kigaidi.

Siku ya tukio Sir David alikuwa ameenda katika Kanisa la Belfairs Methodist kukutana na wananchi wake anaowawakilisha wa eneo la Southend West ambapo alikua anatarajia kufanya mkutano pamoja nao kabla ya kushambuliwa.

> Mbunge auawa kwa kuchomwa kisu

Sir David ni Mbunge wa pili kuuawa akiwa bado anahudumu katika miaka mitano iliyopita na kufuatia mauaji ya Mbunge Jo Cox mnamo 2016. Kutokana na tukio hilo kijana mmoja Muingereza mwenye asili ya Kisomali anaejulikana kama Ali Harbi Ali mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa kwa kuhisiwa kuhusika na tukio hilo la mauaji.

error: Content is protected !!