Kijana Mtanzania alivyouawa kwa risasi Marekani

HomeKimataifa

Kijana Mtanzania alivyouawa kwa risasi Marekani

Kijana wa Kitanzania, Humphrey Magwira mwenye umri wa miaka 20, ameuawa kikatili kwa kupigwa risasi na kufariki papo hapo.

Humphrey alikuwa akiendesha gari kuelekea sehemu ya kukata nywele “Barber Shop”, bahati mbaya alipata ajali ndogo ya kugonga gari nyingine ambapo aliyegongwa alitoka bila maelezo na kumpiga risasi kadhaa na hatimaye Humphrey kukata kauli papo hapo.

Humphrey na familia yake walikwenda Marekani akiwa na umri wa miaka 11. Mama yake mzazi Josephine Kuyangana na Baba yake Exuperius Magwira wanasema kuwa walienda Marekani wakidhani wangepata amani, lakini imekuwa kinyume chake. Huku akilia kwa uchungu Mama mzazi wa Humphrey alisema kuwa kijana wake alikuwa mchapa kazi, aliyependa kusoma na michezo.

Humphrey hadi umauti unamkuta alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Houston akisome masomo ya Uhandisi wa Kompyuta huku akifanya kazi za mafunzo kwa vitendo (field internship) kupitia kada anayosomea.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo aitwaye, Ramon Vasquezhas mwenye umri wa miaka 19, anashikiliwa na jeshi la Polisi kw makosa ya mauaji, huku bondi ya dhamana ikitajwa kuwa shilingi bilioni 1.15 kwa fedha za Kitanzania.

Wazazi wa Humphrey wanafanya taratibu za mazishi na wanaazimia mtoto wao mpendwa kuzikwa nyumbani Tanzania ambapo hivi sasa wanatafuta michango kutoka kwa wadau mbalimbali kufanikisha hilo.

error: Content is protected !!