Faida  5 za kutoa Ushuzi

HomeElimu

Faida 5 za kutoa Ushuzi

Watu wengi wamekua waoga sana kutoa ushuzi wakidhani kwamba wanakosea hivyo wanaamua kubana hewa hiyo chafu ndani yao bila kujua kwamba kiafya ni vyema ukajiachia ili hewa hiyo iweze kutoka nje. Unapaswa kufahamu kufanya hivyo sio jambo jema kwa afya na ni bora ukaenda sehemu ya faragha ili usiwaudhi watu wengine.

Zifuatazo ni faida 5 za kutoa ushuzi

1. Afya kwa utumbo wako
Wazazi wamekua wakiwaambia watoto wao kutojibana pindi wapatapo ushuzi, jambo hili ni kweli kwani unapojibana na kama una matatizo ya kwenye mfumo wa chakula basi itakuletea shida ni vyema ukaachia hewa hiyo chafu itoke.

2. Hupunguza kujaa kwa tumbo na maumivu
Endapo utakuwa unatoa ushuzi basi hapa utapunguza kujaa kwa tumbo au kuvimba na maumivu yanayotokana na gesi hiyo chafu.

3. Harufu ya ushuzi ni kinga
Ni vyema ukawa unatoa ushuzi kwani hewa ile ni gesi ya “hydrogen sulphide” ambayo utakapoinusa basi itakupunguzia hatari ya magonjwa kwani harufu ya ushuzi inaweza kukuepusha na magonjwa ya mshtuko wa moyo na kiharusi.

              > Utafiti: Harufu mbaya ya ushuzi inazuia Kansa, magonjwa ya akili

4. Husaidia kujua kama unakula mlo kamili
Gesi utakayoitoa kwenye ushuzi itakupa mwongozo wa kujua kama unakula chakula kamili kwani endapo utakua unatoa ushuzi wenye harufu sana basi ni ishara kwamba haupati mlo kamili hivyo ni vyema ukaanza kula mlo kamili.

5. Kuupa mwili unafuu
Unapotoa ushuzi mwili unakua umepata unafuu kwani wengi huwa wanabana ushuzi bila kujua kwa kufanya hivi unakua unaubana mwili, na mara nyingi watu hufanya hivi kwa kuhofia kuonwa na watu.

Hivyo basi ni vyema ukawa unatoa ushuzi ili kuwa na afya na kuepeuka maradhi madogo madogo.

error: Content is protected !!