Utafiti: Harufu mbaya ya ushuzi inazuia Kansa, magonjwa ya akili

HomeElimu

Utafiti: Harufu mbaya ya ushuzi inazuia Kansa, magonjwa ya akili

Pale unapohisi hali ya tumbo kujaa “gesi”, suluhu pekee huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo. Habari njema kwa mujibu wa wanayansi toka Chuo Kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, kitendo cha kujamba japo kinachukiza na kukera lakini kina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.

Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata pengine saratani.Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.

Watu wengi wameonesha kushangazwa  ana utafiti huu kwamba eti harufu mbaya inayotokana na mtu kujamba inaweza kuzuia magonjwa fulani mwilini kama vile saratani.

Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.

“ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kujamba, hutengenezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa fulani, ’’amesema Daktari Mark Wood, Profesa wa chuo hicho.

Pamoja na manufaa yanayoelezwa, kwa mujibu wa utafiti huo, angalizo limetolewa kuwa gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kujamba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu kupatwa na magonjwa kama vile, saratani, kiharusi, mshtuko wa moyo na kuumwa na mifupa.

error: Content is protected !!