Tetesi za soka Barani Ulaya Ijumaa 17.09.2021: Benitez, Arteta, Ginter, Rudiger, Pogba, Werner

HomeMichezo

Tetesi za soka Barani Ulaya Ijumaa 17.09.2021: Benitez, Arteta, Ginter, Rudiger, Pogba, Werner

Kocha wa Everton Rafael Benitez amepatia kipaumbele kumsajili beki wa kati katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Football Insider)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anatarajiwa kumpandisha kiungo wa kati wa timu ya wachezaji chipukizi katika klabu hiyo Charlie Patino katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku kukiwa na ripoti kwamba klabu ya Barcelona inamnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 wa England. (Mirror)

Barcelona ina matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao iwapo mchezaji huyo (28) ataamua kutotia saini kandarasi mpya na Man United, ijapokuwa watakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka klabu za PSG, Juventus na Real Madrid. (Fichajes – Spanish)

Kocha msaidizi wa Newcastle Graeme Jones na mshambuliaji wa England Dwight Gayle (30) walirushiana maneno makali katika uwanja wa mazoezi huku nahodha Jamaal Lascelles akilazimika kuingilia kati na kuwatawanya wawili hao. (Mail)

Kandarasi ya beki wa Ujerumani Antonio Rudiger katika klabu ya Chelsea inakamilika msimu ujao na mazungumzo ya kuiongeza yamegonga mwamba. (Times – subscription)

Baadhi ya wanachama wa bodi ya klabu ya Barcelona wamemtaka rais wa klabu hiyo Joan Laporta kumfuta kazi kocha Ronald Koeman baada ya kulazwa 3-0 na Bayern nyumbani. (AS Spanish)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner (25) ni miongoni mwa wachezaji wanne wanaonyatiwa na Borussia Dortmund iwapo mshambuliaji matata wa klabu hiyo Erling Halaand ataondoka katika klabu hiyo msimu ujao. (SportBild – German)

Tottenham ipo mbioni kumsajili mchezaji wa Borussia Monchengladbach Matthias Ginter lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich na Real Madrid ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Ujerumani. (Calciomercato – Italian)

 

error: Content is protected !!