Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 06 (Xavi mbioni kuinoa Barcelona, Franck Kessie Kuziba pengo la Pogba Man United)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 06 (Xavi mbioni kuinoa Barcelona, Franck Kessie Kuziba pengo la Pogba Man United)

Klabu ya Red Bull Salzburg wanahitaji kati ya pauni milioni 25 – 34 kumuuza mshambuliaji wa Ujerumani Karim Adeyemi, ambaye anawindwa na klabu ya Liverpool na Bayern Munich (Sky Germany).

Rais wa Real Madrid Florentino Perez ana matumaini Mshambuliaji wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe 22, atajiunga na klabu hiyo mwaka 2022 (El Debate – Spanish).

Fiorentina imesema mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, anayehusishwa na kuhamia Arsenal na Tottenham, hajakubali mkataba mpya na klabu hiyo ya Serie A (Evening Standard).

Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa AC Milan Franck Kessie 24, kama mbadala wa Paul Pogba iwapo ataondoka dirisha dogo la usajili kunako Januari (Calcio Mercato – Italian).

Liverpool bado wana nia ya kumsajili mchezaji wa Torino Bremer 24, lakini pia anahusishwa na klabu za Manchester United na Manchesyer City zimekuwa zikimfuatilia Mbrazili huyo (Calciomercato – TEAMtalk).

Mlinda mlango wa Ajax na Cameroon Andre Onana 25, yupo tayari kujiunga na Inter Milan kama mchezaji huru mwaka 2022 (Fabrizio Romano).

Beki wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger 28, amesema hatetereshwi na tetesi zinazomhusisha yeye na Bayern Munich (Mirror).

Wakati mkataba wa Rudiger ukitarajiwa kuisha muda wake mwisho wa msimu ujao, kocha wa Chelsea Thomas Tuchel anatamani mlinzi huyo wa kati asaini mkataba mpya huku mahasimu wao Tottenham wanamnyatia kwa ajili ya uhamisho huru (Express).

Juventus wanajiandaa kuachana na kiungo wao Weston McKennie, ambaye anafuatiliwa na Tottenham na West Ham (TEAMtalk).

Barcelona ipo kwenye mazungumzo na Xavi (41), aliyekuwa kiungo wa katika klabu hiyo, achukue nafasi ya kocha Ronald Koeman, lakini makubaliano yao na Mhispania huyo bado hayajafikiwa (90min).

error: Content is protected !!