CHADEMA kupokea milioni 102 ya ruzuku kwa mwezi

HomeKitaifa

CHADEMA kupokea milioni 102 ya ruzuku kwa mwezi

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema chama hicho kimekubali kupokea ruzuku ya Sh. milioni 102 kwa mwezi.

Ikiwa chama hicho kitapokea kiasi hicho cha fedha, kitapata zaidi ya Sh. bilioni 2.9 ambayo ni ruzuku kwa kipindi cha kuanzia Novemba 2020 hadi Machi mwaka huu.

Lissu alitoa kauli hiyo wakati akiulizwa maswali na wananchi mbalimbali kwenye mtando wa Club House jana na kufafanua kuwa fedha hizo wameanza kuzipata mwezi huu na wameahidiwa kulipwa malimbikizo yote ya nyuma.

“Tulijulishwa katika kikao cha Kamati Kuu kwamba ruzuku imeanza kulipwa kwa mara ya kwanza mwezi huu kwa kulipa malimbikizo ya nyuma, haijalipwa yote lakini imeanza kulipwa.

error: Content is protected !!