Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 10 (Pogba kutimkia Juventus, huku Newcastle ipo mbioni kumalizana na Steve Bruce)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 10 (Pogba kutimkia Juventus, huku Newcastle ipo mbioni kumalizana na Steve Bruce)

Klabu ya Juventus ina nafasi kubwa ya kumsajili Paul Pogba, ambaye mkataba wake na Manchester United upo mbioni kuisha, kama watafanikiwa kuwauza wachezaji wawili ili wapate nafasi ya kumsajili nyota huyo (La Gazzetta dello Sport).

Beki wa Burnley James Tarkiwski (28) ni mmoja wa wachezaji wa kwanza atakayeanza kusajiliwa na Newcastle, huku klabu hiyo ikiwa ikimfuatilia Jesse Lingard 28, kiungo mshambuliaji huyo anayetarajiwa kumaliza mkataba wake na klabu ya Manchester United msimu ujao majira ya kiangazi (Sunday Telegraph).

Klabu ya Newcastle pia inavutiwa na mshambuliaji wa Paris St-Germain, Mauri Icardi (28) ingawa klabu za Tottenham na Juventus pia zinamtolea macho mchezaji huyo (Calciomercato, Mail on Sunday).

Wamiliki wapya wa Newcastle wanajiandaaa kumfuta kazi kocha Steve Bruce wiki ijayo (Sunday Mirror).

Newcastle United vilevile inaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa kati wa Napoli Kalidou Koulibaly, 30 (Football Insider).

> Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 09 (Kane na Mbappe Newcastle, huku Van de Beek akielekea Barcelona)

Liverpool inafuatilia kwa karibu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Ousmane Dembele kwa uhamisho huru ambapo mkataba wa mchezaji huyo na Barcelona ukielekea kuisha mwisho wa msimu huu wa 2021/22 majira ya kiangazi (Teamtalk).

Klabu ya Inter Milan inamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette (30) na mshambuliaji wa Real Madrid Mserbia Luka Jovic (23) kama machaguo ya mwezi Januuari (La Gazzetta dello Sport).

Leeds United wanaamini kuwa kiungo wao Kalvin Phillips ataongeza mkataba wake na klabu hiyo kabla ya mwisho wa mwaka, wakati mazungumzo yakiwa kwenye hatua za mwisho (Football Insider).

Sevilla waaangalia uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Blackburn Rovers na Chile Ben Brereton 22, huku mshambuliaji wa klabu hiyo Yorsef En-Nesyri 24, akihusishwa na kujiunga Arsenal au Tottenham (Teamtalk).

Klabu ya Manchester United inajiandaa kuanza mazungumzo na beki wa kati wa England Harry Maguire (28) kuboresha masharti ya mkataba wa mchezaji huyo (Sunday Mirror).

error: Content is protected !!