Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 09 (Kane na Mbappe Newcastle, huku Van de Beek akielekea Barcelona)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 09 (Kane na Mbappe Newcastle, huku Van de Beek akielekea Barcelona)

Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Demba Ba 36, amejitolea kuichezea klabu hiyo mpaka pale atakapostaafu baada ya klabu hiyo kuuzwa (Star).

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anaweza kukataa kuchukua nafasi ya Steve Bruce kunako klabu ya Newcastle (Sun).

Newcastle inakadiriwa inaweza kutumia hadi pauni milioni 190 mwezi Januari bila kuvunja sheria za Play Fair, kuwanunua mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane (28) na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe (22) wakiangalia upatikanaji wao (Telegraph).

Kiungo wa kati wa Barcelona, Philippe Coutinho (29) anaweza kuelekea Newcastle United ifikapo januari kwenye dirisha dgo la usajili (Sport- Spanish).

> Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 08 (Lampard na Gerrad kuchukua mikoba ya Bruce kunako Newcastle, Asensio kujiunga na Liverpool)

Kiungo wa Man United Bruno Fernandes (27) amekuwa akiwasiliana na nyota wa Leeds, Raphinha (24) kuhusu uwezekano wa yeye kuhamia Manchester United (Mirror).

Beki wa kati wa Ujerumani Antonio Rudiger (28) ndiye chaguo la kwanza la uhamisho wa Real Madrid mwaka ujao, huku mkataba wa mchezaji huyo wa Chelsea unaisha mwisho wa msimu huu (ABC, Mail).

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anasita kumruhusu Van de Beek aondoke Manchester United ifikapo Januari na atazuia hatua yoyote itakayohusiha kumuuza (ESPN).

Klabu ya Barcelona wanahitaji huduma ya Donny van de Beek (24) na mchezaji wa Tottenham Tanguy Ndombele (24) ambao wote ni moja ya wachezaji wawili kati ya wane wanaohitajika Nou Camp (Sport – Spanish).

Kiungo wa kati wa England Ainsley Maitland-Niles (24) na kiungo wa Misri Mohamed Elneny (29) wanaweza kuondoka Arsenal kwenda kutafuta nafasi zakucheza katika klabu nyingine baada ya nafasi zao katika kikosi cha kwanza kusua sua (Sun).

Mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero 33, alikataa kuhamia Juventus kabla ya kujiunga na Barcelona kwa uhamisho wa bure baada ya kuondoka Manchester City msimu uliopita (Sport- Spanish).

Klabu ya Juventus ina mpango wa kumuuza kiungo wa Wales Aaron Ramsey 30, mnamo dirisha dogo la usajili Januari, huku akihusishwa na klabu za West Ham na Everton (Calcio Mercato – Italian).

error: Content is protected !!