Kamanda Muliro azungumzia sakata la Kizz Daniel

HomeKitaifa

Kamanda Muliro azungumzia sakata la Kizz Daniel

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ameeleza hatua za Jeshi la Polisi kuhusu sakata la Msanii kutoka nchi Nigeria, Kizz Daniel kushindwa kufanya onyesho kwenye tamasha la Summer Amplified.

Kamanda Muliro amesema kwamba walimkata Kizz Daniel kwa ajili ya mahojiano na kuweza kubaini changamoto ya mikataba jambo alilosema linafanyiwa kazi kisheria zaidi.

Pia amesema, kwa namna sakata hili lilivyo ni lazima sheria itumike na si kukurupuka ili kuweza kurudisha haki ya waandaji wa tamasha hilo mashabiki ambao walinunua tiketi kwa gharama.

“Unajua hili suala lilivyokaa sio la kipolisi pekee, kuna mambo ya mikataba hivyo tunashirikiana na vyombo vingine vya kisheria.

“Tunafanya hivyo kila upande uweze kupata haki yake kwani ujio wake hapa kuna watu wamemleta na wamemlipa, kwa hiyo nadhani unavyoona lilivyokaa sio suala la kushughulikiwa na taasisi moja,”amesema Muliro.

 

error: Content is protected !!