Aliyepandikizwa moyo wa nguruwe afariki

HomeKimataifa

Aliyepandikizwa moyo wa nguruwe afariki

David Bennett binadamu wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa upandikizwaji wa moyo wa nguruwe amefariki dunia Machi 8 mwaka huu, David amefariki akiwa na umri wa miaka 57 ikiwa ni miezi miwili tangu afanyiwe upasuaji huo Januari 7 mwaka huu.

David alifanyiwa upasuaji nchini Marekani katika hospitali ya University of Maryland Medical, baada ya idhini kutolewa na wasimamizi wake kutokana na hali mbaya aliyokua nayo.

David alikua hana uwezekano wa kuishi tena kama asingefanyiwa upasuaji huo ndipo wakaamua kutumia moyo wa nguruwe kunusuru maisha yake.

Baada ya upasuaji huo David alipata ahueni katika siku za mwanzoni na alifanikiwa kujumuika na familia yake kutazama fainali za Super Bowl zilizofanyika Februari 13. Baadaye hali yake ilibadilika na kupelekea kukutwa na umauti.

error: Content is protected !!