Aruhusu wanaodaiwa ada kufanya mitihani

HomeKitaifa

Aruhusu wanaodaiwa ada kufanya mitihani

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Tulia Ackson ameielekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoa tamko la wanafunzi wa vyuo wanaodaiwa kutozuiliwa kufanya mitihani.

“Wabunge wamekuwa wakikutana na watoto wengi ambao wamekuwa wakiwaomba wawasaidie kuwalipia ada kwani asipofanya hivyo haruhusiwi kufanya mitihani,

“Kama amesoma aruhusiwe kufanya mitihani, matokeo yake ndyio yasubiri. Kama ameweza kusoma darasani na yeye amejiandaa kwa ajili ya mtihani akitaraji mzazi wake ataweza kulipa wakati anaingia kwenye mtihani, hatua ya kumzuia kunamuweka kwenye mazingira magumu hawezi tena kufikiri mtihani,” alisema Spika Tulia.

Aidha, alisisitiza pia kuhusu sare za shule za shule za msingi ziangaliwe kwa kuruhusu kila maeneo kuweka utaratibu na sababu ya rangi hizo.

“Sare kwa wanafunzi wa shule za msingi ni shati jeupe, sketi na kaptula ya bluu zinahusiana na elimu anayoipata , hizi rangi ni mtihani kwani maji ya baadhi ya maeneo ni changamoto na pia sabuni vijijini ni changamoto,

“Kila maeneo yao kuweka utaratibu, kuna sababu zilizofanya kuweka rangi zile, sasa tukazitazame, unaweza kuliona ninjambo dogo lakini ni kubwa sana kwa watoto wa vijijini,” alisisitiza Spika Tulia.

 

error: Content is protected !!